Sunday, 23 August 2015

TAARIFA JUU YA UTATUZI WA SHIDA YA MAKAZI KWA WANACHUO WA MUHIMBILI



YAH: TAARIFA JUU YA HOSTELI ZA ZIADA.
Ndugu wanamuhasso...
Kwanza, tunapenda kuchukua nafasi kuwapongeza kwa mara nyingine tena kwa kumaliza mitihani kwa ujumla wake na kuanza likizo yetu ndefu.
Pili,makala hii ina dhumuni kuu kubwa la kukuhabarisha hatua iliofikiwa na Serikali ya wanafunzi ,MUHASSO juu ya ufuatiliaji wa kero ya Makazi Chuoni kwetu,tunapenda kutoa taarifa tu ya awali juu ya maswala ya ufuatiliaji wa hosteli mpya za ziada na za bei inayowezekana kulipwa na Wanafunzi kama ilivyokuwa katika ahadi zetu za Kiutumishi katika uongozi wetu wa Mwaka 2015/16.
MUHASSO  kwa kushirikiana na ofisi ya SSB ilifanya matembezi ya kutafuta hosteli mpya katika maeneo tofauti tofauti ikiwemo Kariakoo[Fire] kwa ukaribu zaidi na maeneo ya Lumumba.
Lakini pia tulikaa na kuongea na wamiliki katika hostel hizo za Karikoo na Lumumba kisha kukubaliana nae ili kuona bei anayoweza kututoza kwa mwezi. Mpaka kikao kinaisha tulikuwa tumefikia kiasi cha TSH 60,000 na yeye akiwa TSH 65,000 kwa kitanda kimoja  hivyo kubaki hapo na kusema tutaliangalia tena na kukaa mezani tena.
[chumba kimoja kina deka - vitanda viwili au vitatu]
Baada ya hapo, tunategemea kupeleka swala hili katika meza ya mazungumzo  na MUHAS kwa maana ya menejimenti ya CHUO ili tuone ni kwa  namna gani aidha Chuo ama Mamlaka zingine zinaweza kutusaidia japo kuchangia gharama hizo ili zisituumize sana wanaMUHASSO.
Habari za zaidi kuhusu swala  hili zitazidi kuwajia hapa hapa na hivyo tunaombwa  kujitahidi kutembelea hapa mara kwa mara  na  kuwapasha habari wengine ili wafahamu kinachoendelea.
Mwisho, pongezi za dhati ziwaendee viongozi wa Ofisi kuu na Wizara ya Makazi kwa utumishi wao  wa hali na mali katika hatua zote za kulitafutia ufumbuzi tatizo hili.
Kwa niaba ya MUHASSO, tunazidi kuwatakia likizo njema na afya njema uko mliko.
Kwa mwenye Ushauri na Maoni ya Namna yoyote ile anaweza pia kushauri kupitia ukurasa huu ama njia ambayo itampendeza yeye binafsi.
Mazingira mazuri na safi ya kujisomea ni pamoja na upatikanaji wa Malazi na Makazi ya kuaminika kumwezesha Mwanafunzi kukabiliana na masomo.

Imetolewa na:
Wizara ya Habari ,MUHASSO kwa Niaba ya Wizara ya Makazi,MUHASSO

7 comments:

  1. Hongera kwa jitihada.
    Hizo gharama ni kwa kichwa? Gharama zote zinajumuisha maji na umeme?

    ReplyDelete
    Replies
    1. NDIO.
      NI KWA KICHWA KIMOJA NA ZINAJUMUISHA MAJI NA UMEME

      Delete
  2. Huu ndo uongozi tunao utaka.

    ReplyDelete
  3. Ni safi hii wakuu ila ni vyema na mashart tuyajue ndio tutatoa wazo zaid. Labda tunaruhusiwa kuingia jikoni

    ReplyDelete
  4. Ni safi hii wakuu ila ni vyema na mashart tuyajue ndio tutatoa wazo zaid. Labda tunaruhusiwa kuingia jikoni

    ReplyDelete
  5. 🙌🙋🙌🙌🙌🙌

    ReplyDelete
  6. mpaka sasa kuna nini kinaendelea
    mtutaarifu tusije kulala nje.

    ReplyDelete