Wednesday, 2 September 2015

MAAZIMIO YA KIKAO CHA SUEC CHA TAREHE 02/09/2015

YAH: KIKAO CHA SUEC JUU YA MATOKEO.
Habari ndugu wanamuhasso...
Leo, tulikuwa katika kikao cha senate of undergraduates committee (SUEC) ambacho kinadiscuss na kuruhusu matokeo kwenda kikao cha juu (university sénate).
Tumejadili matokeo yote ya shule zote na mambo kadha wa kadha yamepatiwa ufumbuzi na mengine kupelekwa kikao cha juu ili yapate majibu na uamuzi toka huko.

BASIC SCIENCES
Kwa mwaka wa kwanza na wa pili, swala la utata wa kikanuni aliopelekea kutokea na disco kadhaa kwa shule mbalimbali umejadiliwa vizuri baada ya kupewa muda wa wawakilishi wa wanafunzi kutoa maelezo na hatimaye SUEC imekubaliana na wanafunzi na kupendekeza kuwa sheria ya GPA 1.6 iwe ndiyo kipimo cha mwanafunzi kuruhusiwa kuendelea au kutoendelea na shule. Kwa hiyo SUEC imeandika kama mojawapo ya mapendekezo yake kuwa kipengele cha sup 3 kisitumike na badala yake wanafunzi wote wenye GPA 1.6 na zaidi waruhusiwe kufanya supplementary exams.
Aidha, tunasubiri Senate itakayofanyika siku ya jumatatu ya tarehe 7 mwezi huu itoe maamuzi ya mwisho juu ya suala hili.
CLINICAL YEARS
Kwa wanafunz wa clinical years kumekuwa na swala la muda wa ufanyaji wa sup za rotations kipindi cha likizo.
Hoja hii tuliijadili kwa muda baada ya kuiweka mezani na hatimaye SUEC ikaamua turudi katika ngazi ya shule tukazungumze tena na Shule ya kidaktari ili tufikie maelewano mazuri.
Pia, napenda kuwapongeza wote waliohitimu na kufaulu bila kupata sup na nawatakia mema huko mbele.
Kwa finalists waliopata sup nawatakia mema ili muweze kufanya na kufaulu ili muweze kuendelea.
Napenda kwa nafasi ya kipekee, kumshukuru wazir wa Elimu na viongoz wa shule kwa ushiriki mkubwa Wa kufanikisha yote ya kuwasaidia wanafunzi wenzetu.
NOTE:
Yeyote atakayetafutwa naomba atoe ushirikiano mkubwa kwa viongoz ili tufanikishe jambo lake mapema.
Imetolewa na:-
Ofisi ya rais - MUHASSO.
02.09.2015.
Rais wa MUHASSO 2015/16, Ndugu Mathew Mandawa

No comments:

Post a Comment