YAH: TAARIFA JUU YA
MASWALA YA PROSPECTUS NA MATOKEO.
Ndugu wanamuhasso,
Hivi karibuni kumekuwa na maswali mengi juu ya prospectus yetu
na matokeo ya mitihani yetu ya mwisho wa Semista ya pili na hivyo kuleta
mkanganyiko miongoni mwetu.
MUHASSO, kupitia ofisi ya Rais na wizara ya elimu na
viongozi wa Shule tano zilizopo inaendelea kulishughulikia
hili na itatoa majibu yake kwa ufafanuzi zaidi kila mara baada ya kila kikao/vikao
kuisha katika levo zifuatazo,nazo ni:-
1: Shule [School boards]
2: Seneti ya wanafunzi wa digrii
[SUEC]
3: Seneti kuu [University
Senate].
Mpaka leo hii 24/8/2015, ni shule mbili zilizokuwa zimekaa
vikao vyake na kupitisha matokeo yalio na utata na shule ya uuguzi kubandika
matokeo hayo yaliyoibua maswali lukuki miongoni mwetu.
Hivyo,sisi kama MUHASSO tunawasihi tuwe wastahimilivu kwa siku kadhaa ili kuruhusu shule zingine kupitisha matokeo yao na hatimae kuweza kupata matokeo ya pamoja, na hapo baadae sisi kama MUHASSO kutoa taarifa zaidi juu ya matokeo na utata uliopo katika
prospectus yetu.
Pia , ifahamike kuwa MUHASSO imekuwa ikilihoji swala hili
toka lilipoanza kuleta madhara kwetu mwezi February,2015 na kuliandikia waraka
wa maombi na mapendekezo ya wanafunzi ili japo lisitumike kama lilivyo ili
kuepusha ukomo wa masomo [Discontinuation] kwa baadhi ya wanafunzi ambao kwa namna moja amanyingine hawakua na ufahamu juu ya kipengele kipya ndani ya Prospectus.
Serikali hii inaendelea kwa ukaribu kulifuatilia hili
swala,hasa kwa kulihoji na kushinikiza kuibua mijadala katika vikao vyote tunavyokuwa na uwakilishi wa wanafunzi
huko. Yeyote atakae ona matokeo yake kisha akaona utata au kutoridhika awataarifu
viongoz wake wa shule husika mapema mapema zaidi ili na sisi tuweze kulifuatilia mapema na kwa uzito linalostahiki.
Mwisho, tunawashukuru
viongozi wa ofisi kuu, wizara ya Elimu na viongozi wa Shule kwa
utumishi wao katika hatua zote za kulitafutia ufumbuzi tatizo hili.
Kwa niaba ya MUHASSO, tunazidi kuwatakia likizo njema na
afya njema popote mlipo.
Imetolewa na:
Wizara ya Habari ,Kwa niaba ya ;
OFISI YA RAIS,MUHASSO
Wizara ya Habari ,Kwa niaba ya ;
OFISI YA RAIS,MUHASSO
good work, keep it up
ReplyDelete