Tuesday, 7 June 2016

RIPOTI YA SERIKALI YA WANAFUNZI, MUHASSO 2015/2016.



 MUHIMBILI UNIVERSITY OF HEALTH AND ALLIED SCIENCES STUDENTS’  ORGANISATION
                                               MUHASSO
                   SERIKALI YA WANAFUNZI, MUHASSO 2015/2016.

       RIPOTI YA SERIKALI YA WANAFUNZI, MUHASSO 2015/2016.

Ndugu  WanaMuhasso..
Kwanza, Napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema yake ya uhai na pumzi anayotupa mpaka saa hii unasoma ripoti hii ya serikali ya wanafunzi, MUHASSO.

Tukiwa tunafika mwishoni mwa dhamana ya uongozi mliotupa kwa kura zenu ili kuiongoza taasisi yetu ya jumuiya ya wanafunzi, MUHASSO.  Binafsi kama rais napenda niwakumbushe kidogo na kutoa mrejesho wa kazi mlionipa kwa mwaka mmoja kama kiongozi wenu katika utumishi wa kuiongoza Jumuiya hii ya wasomi.


SABABU ZILIZONISUKUMA KUGOMBEA URAIS WA MUHASSO 2015 – 2016.
Hii ni kuwakumbusha wanaMuhasso wote walioniamini na kunipigia kura hata wale ambao hawakunipigia kura ila walinipa ushirikiano baada ya kutangazwa mshindi 18/4/2015 kuwa rais mpya wa serikali ya wanafunzi, MUHASSO.
Zifuatazo ndizo sababu zilizonisukuma kama mmoja wa wanamuhasso lakini kwa wakati huo nikiwa waziri wa mahusiano, sera, utawala bora, jinsia na mambo ya nje katika serikali ya rafiki yangu katika siasa na uongozi Rais wa awamu ya kwanza- MUHASSO mpya.
1: Muono wangu na falsafa ninayoiamini  juu ya Muhasso mpya itakayokuwa na umoja na hivyo kuipa nguvu serikali ya wanafunzi, MUHASSO ili kwa kushirikiana kutatua changamoto mbalimbali zilizokuwa zinatukabili. Na hapo ndipo nilipokuja na motto wa “Solidarity Forever…”
2: Kiu ya mabadiliko katika mifumo ya serikali ya wanafunzi, MUHASSO na uendeshaji wa shughuli zake za kutetea, kusimamia na kuwasemea kwa niaba kama daraja kwa utawala wa chuo ili kuhakikisha ustawi wa kila mwanamuhasso unalindwa na kuheshimiwa.
3: Sifa za kiuongozi na uongozi binafsi nilizotaka kuzitumia ili kutumikia jamii ya wasomi wenazangu. Kujiamini, ukweli, ujasiri, uelewa binafsi, kujitoa na upendo kwa watu ni kati ya sifa zilizonisukuma kuzitumia katika nafasi hii kubwa ya utumishi katika serikali.    
Kutokana na sababu hizo ndipo pamoja na mgombea mwenza wangu, Mr Adam Likiliwike tukaingia katika kinyang’anyiro cha kugombea na kwa sapoti toka kwa rafiki na wanafamilia wa Muhasso tukafanya kampeni tukiwa na sera zetu zifuatazo ambazo zilitupa kuaminika na kushinda uchaguzi huo na kuapishwa 24/04/2015:-
SERA 1: Kuunda serikali ya umoja yenye uwakilishi wenye uwiano na kupunguza gharama ya uendeshaji wa serikali.
·         Kuunda serikali yenye kujali uwiano wa kishule, kikozi, kidarasa na kijinsi.
·         Kuondoa/kupunguza  gharama zisizo na ulazima za kuendesha serikali kwa kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri.
SERA 2: Kuweka mifumo yenye tija katika maswala ya Elimu.
·         Ushiriki wa Serikali ya wanafunzi katika uundwaji wa Prospectus na Almanac ya Chuo na kutupa uwakilishi wa kuwasilisha maoni na mapendekezo yetu.
·         Kuweka mazingira stahiki ya kusomea na kujifunza ikiwemo kufuatilia utengenezaji wa vifaa kazi kama maiki, spika, projectors na mazingira bora kusomea katika maeneo ya NLHs, 24 Halls na Library kwa kuhakikisha uwepo wa soketi zinazofanya kazi, feni/AC katika vyumba vya mikusanyiko,
·         Kuondoa tatizo la mwingiliano wa ratiba iliyopelekea wanafunzi kusoma kwa shida pale wanapolazimika kuhama au kuhairisha vipindi wengine wanapohitaji darasa.
·         Kuhakikisha matokeo yanatolewa mapema zaidi na kuwekwa katika mfumo ulio imara wa SARIS inaweza kuonyesha alama Sahihi na GPA ya kila mwanafunzi.
·          Kuhakikisha umalizikaji wa urekebishaji wa viwango vipya vya fedha ya mahitaji maalumu viendane na mahitaji na kuanza kutumiwa rasmi na sisi.
·          Kuweka mpango bora unaofaa wa namna ya kulipia na kufuatilia utunzaji wa nguo zetu za upasuaji(Theatre Attire).
·         Kufuatilia ufanyaji wa mitihani ya marudio(Supplementary) kwa wanafunzi wa mwaka wa watatu, wanne na watano kipindi cha likizo ndefu ya 2015.
SERA 3: Marekebisho ya mfumo wa kufuatilia na kuratibu maswala ya Mikopo na Ruzuku.
·         Kuanzisha mfumo mpya wa kusaini wenye kutumia muda mfupi bila kuathiri ratiba zetu za kimasomo.
·         Kufuatilia kwa kina na ukaribu sio kuulizia ili kuhakikisha pesa zinawafikia wanafunzi kwa wakati. Hii itaenda sawia na kusaini mapema hata kabla ya siku 70 kuisha ili kufanikisha kupata pesa kwa wakati.
·         Kufuatilia taratibu za usainishwaji wa wanafunzi wapatao ruzuku ili kuondoa sintofahamu juu ya wanaostahili kupewa ruzuku ili kuondoa maswali ya wafaidika.
·         Kushirikiana na Chuo na  wanafunzi wote waliokosa mikopo ili waweze kupatiwa mikopo yao katika mwaka mpya wa masomo 2015/2016.

SERA 4: Usimamizi mzuri wa maswala ya huduma za chakula(Cafeteria) na uboreshwaji wa huduma za Afya.
·         Uhusika wa karibu wa serikali ya wanafunzi, MUHASSO katika upatikanaji wa mtoa huduma wa Cafeteria. (Tenderer)
·         Kusimamia kwa makini mikataba wa mtoa huduma ili kuhakikisha huduma bora, yenye usafi na ya gharama nafuu inatolewa kwa wanamuhasso na hii itakwenda sambamba na kuwepo kwa timu maalum ya wanamuhasso watano  watakaokuwa wanasimamia kikamilifu(Food Testors).
·         Kuondoa foleni Chole kwa kuwa na sehemu mbili za kutolea huduma ili kutokuwa na upotezaji wa muda katika foleni za kupata huduma hizo.
·         Kuwepo kwa kadi za Bima ambazo haziishi muda wake kabla ya zingine kutoka na kugawiwa kwa wanafunzi na hivyo kuhakikisha tarehe ya kufikia mwisho(Expiry date) kusogezwa mbele ili kumpa mtumiaji uhuru wa kutumia popote wakati wowote ili kutomlazimu kutibiwa MNH pekee kipindi cha mwanzo
SERA 5: Uboreshaji wa huduma za makazi na Usalama kwa wanafunzi.
·         Utafutaji wa hosteli mbadala zenye gharama nafuu ili kupunguza uhaba wa makazi miongoni mwa wanaMuhasso na hii itakuwa sambamba na kuuomba utawala wa chuo kutuchangia kidogo ili kutomuumiza mwanafunzi kwa malipo makubwa.
·         Ufuatiliaji wa matengezo ya hosteli zetu kufanyika kwa wakati ili kuweka mazingira salama kwa wanamuhasso.(milango, mapazia, komeo,vioo, viti, meza)
·         Kuhakikisha usafi unafanyika kikamilifu ndani na nje ya hostel ili kufanya wanamuhasso kuishi katika mazingira safi kwa afya zao.
·         Usalama, kuhakikisha kunakuwepo kwa vifaa vya zima moto(functional fire extinguishers) na  wakazi wa hosteli wanapatiwa mafunzo ya kuzima moto.
SERA 6: Kuamsha ari ya ushiriki wa wanamuhasso katika michezo na Burudani.
·         Kuhakikisha upatikanaji wa vifaa vyote muhimu kwa timu zote ili kuwezesha timu hizo kuwa na mazoezi ikiwemo jezi,mipira, first aid kits. 
·         Kufanyika kwa mechi mbalimbali ndani na nje ya MUHAS, uwepo wa MUHASSO ligi na bonanza za michezo mbalimbali za ndani.
·         Kuandaa      matukio ya ufumbuzi wa vipaji vya wanamuhasso yaani Talents Show.
·         Kutengeneza Pool table ya Chole ili iweze kutumika ikiwa katika ubora wake ili kuwapa wanamuhasso pumziko la kiakili.
·         Kuwepo kwa TV nje ya Cafeteria ili kuondoa msongamano katika ukumbi wetu wa ndani.
SERA 7: Uboreshaji wa mifumo ya kutoa habari, huduma za mitandao na Intaneti(WiFi).
·         Ufualiaji na kuhakikisha uwepo na upatikanaji wa WIFI imara yenye nguvu katika hosteli(Chole na kampusi kuu) zetu na zaidi maeneo ya kusomea(NLHs/24 Hall).
·         Kuimarisha mfumo mmoja wa kiserikali wa utoaji taarifa kupitia njia zote zifaazo kwa kuziimarisha kama vile mbao za matangazo, Muhasso facebook pages, Muhasso blogs, Push - Sms na mitandao ya wasapu.
·         Kuzipa mamlaka wizara mbalimbali kutoa taarifa zake kwa ufanisi pasipo kuingiliwa na ofisi za mamlaka ya usimamizi.
·         Kuhakikisha wanamuhasso wote wananufaika na  huduma zote za vyuo vikuu za mitandao ya simu (University offers) kama vile TIGO. VODA na AIRTEL.

SERA  8: Uimarishaji wa uwekezaji na kuongeza mapato ya serikali ya wanafunzi, MUHASSO.
·         Kuipitia mikataba yote kwa umakini ili tuweze kuitumia kukusanya mapato yetu kikamilifu na kuongeza mapato ya serikali.
·         Kuichukua Muhasso stationery na kuiendesha wenyewe ili kupunuza gharama za serikali kununua huduma hizo ambazo huleta gharama kubwa kwa serikali.
·         Kuanzisha miradi mingine ya kuongeza mapato ikiwemo ufunguaji wa Saloon katika hostel za Chole.
SERA 9: Upatikanaji wa usafiri wa uhakika kwa wanafunzi.
·         Serikali itaandaa proposo mbalimbali kwa mashirika na watu binafsi ili kukusanya pesa kwa ajili ya kununua basi moja kwa kuanzia kwa ajili ya kuhakikisha huduma ya usafiri inapatikana kwa wanamuhasso haswa wakazi wa chole. Serikali itatenga Tsh Milioni kumi(10m) kama kianzia ambayo imetoka katika mradi mmoja wa MUHASSO.
                                    
SERA 10:  Kuimarisha uhusiano wa ndani  na nje wa serikali, MUHASSO.
·         Kuanzisha mfuko maalum wa kusaidia wanafunzi wenye uhitaji wa dharura
·         Kuimarisha ushirikiano na taasisi za ndani za kidini, kijamii na kielimu.
·         Kujenga uhusiano wenye faida za taasisi za nje ya chuo ndani ya nchi na nje ya nchi pia.

MAFANIKIO YA SERIKALI YA WANAFUNZI, MUHASSO 2015/2016.
Ndugu wanamuhasso,
Baada ya kujinadi kwa dhati na kwa kujiamini ili kuweza kuleta mabadiliko makubwa yaliyotegemewa na mamia ya wanamuhasso katika 2015/2016. Yafuatayo yamefanyika na kufanikiwa kama ambavyo niliyaahidi pamoja na Makamu wangu wa rais:-
SERA 1: Kuunda serikali ya umoja yenye uwakilishi wenye uwiano na kupunguza gharama ya uendeshaji wa serikali.
·         Tumefanikiwa kuunda serikali yenye kujali uwiano wa kishule, kikozi, kidarasa na kijinsi sawa sawa na matakwa ya kikatiba na hii imeimarisha umoja na upendo  wetu.
       Ofisi ya rais – MDs
          Ofisi ya waziri mkuu - BPharm na Public health.
          Mawaziri – MDs  5, Bpharm- 1, Public health – 1, BscN-1  and  DDS -1.
          Naibu mawaziri - MDs 9, Bpharm- 3, Public health – 1,BscN-1 and  DDS -1.
·         Tumepunguza ukubwa wa serikali (Executive) kwa nafasi 10 pungufu kulinganisha na ilivyokuwa mwanzo na hii imepunguza matumizi ya pesa za wanamuhasso katika gharama za kuendesha serikali na kuwekeza zaidi katika huduma za pamoja.
SERA 2: Kuweka mifumo yenye tija katika maswala ya Elimu.
·         Serikali imeshiriki kwa kukusanya maoni na mapendekezo toka kwa wanafunzish iriki juu uundwaji wa Prospectus na Almanac LAKINI bado tulikutana na Ugumu katika kuelewana juu ya kuondolewa kwa sheria ya Sapu 3 na muda wa kufanya sapu wakati wa likizo ndefu.(clinical rotations)
Japo sheria hii haijatoweka kabisa lakini imepunguzwa kutotumika kwa  mwaka wa pili wa kozi zote za miaka mitatu ( BMLS, BRRT na BScEnv ).
·         Serikali imehakikisha kuwepo kwa  matengenezo ya vifaa kazi kama maiki, spika, projectors na kuhahakisha mazingira bora kusomea katika maeneo ya NLHs, 24 Hall na Library kwa kuhakikisha uwepo wa soketi zinazofanya kazi na feni/AC.
·         Tumehakikisha tatizo la muingiliano wa ratiba limepungua kwa kiasi kikubwa kulinganisha na hapo awali kwa kuwa na ratiba kuu inayoonyesha madarasa kwa kupishana.(Central timetable)
·         Tumehakikisha matokeo yanatolewa mapema zaidi na imewapa fursa ya kujiandaa kwa mitihani ya marudio (supplementaries) na kuanza mafunzo mapema (internship) kwa waliohitimu.
·          Kuanzishwa kwa mfumo wa kuonyesha GPA ya kila mwanafunzi katika akaunti za ‘SARIS’
·          Tumehakikisha urekebishaji wa viwango vipya vya fedha ya mahitaji maalumu umefika bodi ya mikopo na kufanyiwa kazi katika kipindi cha bajeti 2016/17. Na hii itatoa fursa ya kuanza kutumika kwa mwaka wa kwanza wapya wa 2016/2017.
·          Tumeweka mpango bora wa kulipia na kufuatilia utunzaji wa nguo zetu za upasuaji (Theatre Attire) ambapo wale  mwaka wa tatu pekee ndio watakuwa wanalipia ununuzi wa nguo hizo.
·         Tumefanikiwa kusaidia kufanyika kwa mitihani ya marudio (Supplementary) kwa wanafunzi wa mwaka wa watano(MD5X) kipindi cha likizo ndefu ya oktoba 2015.
SERA 3: Marekebisho ya mfumo wa kufuatilia na kuratibu maswala ya Mikopo na Ruzuku.
·         Tumefanikiwa kuanzisha mfumo mpya wa kusaini wenye kutumia muda mfupi bila kuathiri ratiba zetu za kimasomo.
·         Tumefanikiwa kuhakikisha na kufuatilia kwa kina na ukaribu na kupelekea pesa kuwafikia wanafunzi kwa wakati.
Japo kumekuwa na changamoto kwa bumu la april, 2016 na pesa za disemba, 2015  za BS, SFR na PT zilichelewa kwa sababu zilizokuwa nje ya MUHASSO.
·         Tumefanikiwa kusimamia taratibu za usainishwaji wa wanafunzi wapatao ruzuku na hii imeondoa sintofahamu juu ya wanaostahili kupewa ruzuku.
·         Tumeshirikiana na Chuo na  wanafunzi wote waliokosa mikopo 2014/2015 na wameweza kupatiwa mikopo katika mwaka  2015/2016.

SERA 4: Usimamizi wa maswala ya huduma za chakula(Cafeteria) na uboreshwaji wa huduma za Afya.
·         Serikali, tumefanikiwa kushiriki kikamilifu na karibu katika upatikanaji wa mtoa huduma mpya  wa Cafeteria kwa kulinda maslahi ya wanafunzi wake.
·         Tumemezidi kusimamia kwa makini mkataba wa mtoa huduma ili kuhakikisha huduma bora,usafi na ya gharama nafuu sawaia na mkataba wake  inatolewa.
·         Serikali tumekubaliana na ofisi za NHIF- Ilala juu ya mfumo wa kutoa kadi za Bima wakati tu tunavyofanya usajili chuoni ili kumpa mwanafunzi mtumiaji uhuru wa kutumia popote wakati wowote ili kutomlazimu kutibiwa MNH pekee kipindi cha mwanzo kama ilivokuwa mwanzoni. Kadi zilizopo zitatumiwa mpaka tutakapopata mpya katika mwaka mpya ujao wa masomo.
·         Zaidi, tumehakikisha chanjo dhidi ya homa ya Ini (HEPATITIS VACCINATION) imetolewa kwa wanamuhasso wote waliokuwa tayari.(1209 wamepatiwa chanjo hiyo)
SERA 5: Uboreshwaji wa huduma za makazi na Usalama kwa wanafunzi.
·         Serikali ilifanikiwa kupata hosteli mbadala ili kupunguza uhaba wa makazi miongoni mwa wanaMuhasso lakini muitikio wa wanafunzi ulikuwa mdogo hivyo zikachukuliwa na vyuo vingine.
Japo ,MUHASSO tulifikia hatua nzuri LAKINI juhudi zetu hazikuzaa matunda baada ya chuo kudai hakiwezi kutuchangia gharama ya malazi.ya wanafunzi.
·         Tumezidi kufuatilia matengezo ya hosteli zetu kufanyika kwa wakati ili kuweka mazingira salama kwa wanamuhasso.(milango, mapazia, komeo,vioo, viti, meza)
Japo haijafikia kiwango tulichotegemea kwa sababu zilizotolewa na Chuo kutokuwa na fedha za kukamilisha matengenezo yote HATA HIVYO bajeti ya kutosha imetengwa kwa ajili ya ukarabati huu wakati wa likizo ijayo.
·         Tumehakikisha usafi unafanyika kikamilifu ndani na nje ya hostel ili kufanya wanamuhasso kuishi katika mazingira safi kwa afya zetu.
·         Usalama, tumefanikiwa kuhakikisha wanamuhasso wakazi wa hosteli wamepatiwa mafunzo ya kuzima moto na vifaa vya kuzimia moto vinavyofanya kazi vipo katika hosteli zote.
·         Zaidi, tumefanikisha kuhakikisha ulinzi umeimarishwa haswa baada ya matokeo ya wizi kutokea.
·         Tumehakikisha dawa za kuua wadudu zinapigwa katika hostel zetu na chuo kilitoa ushirikiano mzuri  katika eneo hili.
SERA 6: Kuuhisha ushiriki wa Wanamuhasso katika michezo na Burudani.
·         Tumefanikiwa kucheza mechi mbalimbali ndani na nje ya MUHAS.
·         Tumefanikiwa kuandaa MUHASSO ligi ambapo mwaka wa pili walitwaa kombe
·         Tumefanikiwa kuandaa na kushiriki bonanza za michezo mbalimbali. Mfano: Tigo bonanza
·         Tumeandaa matukio ya ufumbuzi na kuonyesha vipaji vya wanamuhasso yaani TALENTS SHOWs. (Juni,2015 na march, 2016)
·         Tumefanikiwa kununua na kutoa vifaa vyote muhimu vya michezo kwa timu zote ili kuwezesha timu hizo kuwa na mazoezi.(football, volleyball, basketball)
·         Tumetengeneza Pool table ya Chole.
·         Tutakuwa na TV katika Cafeteria ili kuondoa msongamano katika ukumbi wetu wa ndani. (Shukrani kwa mzabuni wetu wa cafeteria, hatua za mwisho zinafanyika ili ifungwe ndani ya Cafeteria yetu).
SERA 7: Uboreshaji wa mifumo ya kutoa habari, huduma za mitandao na Intaneti (WiFi).
·          Tumefanikiwa kuhakikisha uwepo na upatikanaji wa WIFI  yenye nguvu katika hosteli(Chole na M. Campus)haswa maeneo ya kusomea(NLHs/24 Hall/New Cafeteria-Chole).
Japo bado haijawa imara kutokana na uchache wa vifaa unganishi.
·         Tumeonyesha mfano uliosifika katika mfumo wa kiserikali wa utoaji taarifa kupitia njia zote zifaazo kwa kuziimarisha kama vile mbao za matangazo, Muhasso facebook pages, Muhasso blogs, Push - Sms na mitandao ya wasapu na telegram.
·         Serikali imeonyesha mgawanyo wa madaraka kiutendaji kwa wizara mbalimbali kutoa taarifa zake kwa ufanisi pasipo kuingiliwa na ofisi za mamlaka ya usimamizi.
·         Tumesimamia uungwanishaji katika huduma zote za vyuo vikuu za mitandao ya simu (University offers) kama vile TIGO, HALOTEL,VODA na AIRTEL.

SERA  8: Uimarishaji wa Uwekezaji na kuongeza mapato ya serikali ya wanafunzi, MUHASSO.
·         Tumefanikiwa kuipitia mikataba na kusimamia ukusanyaji wa  mapato yetu kikamilifu. Hii imekuwa sambamba na kubadili mtoa huduma katika Saluni yetu ili kuboresha huduma zake.
·         Tumefanikiwa kununua vifaa vyetu wenye vya huduma za kisteshenari na kupunguza gharama za serikali kununua huduma nje.

SERA 9: Upatikanaji wa usafiri wa uhakika kwa wanafunzi.
·         Tumefanikiwa kuandaa proposals na kuzisambaza kwa mashirika na watu binafsi kama vile bank (NMB,CRDB), makampuni ya simu (TIGO, AIRTEL, VODA) na makampuni binafsi (IPPL-Dr. Mengi, QGL- Mr Manji, MeTL- Mr Dewji).
Japo majibu bado sio mazuri mpaka sasa. Ufuatiliaji kwa serikali mpya uendelee.
·         Serikali imekusanya na kutenga Tsh Milioni kumi (10m) kama kianzio ambayo imetoka katika mradi mmoja wa MUHASSO.
                                    .
SERA 10: Kuimarisha Uhusiano wa Ndani  na Nje wa serikali, MUHASSO.
·         Tumefanikiwa kuanzisha mfuko maalum wa dharura kwa ajili ya kusaidia wanamuhasso wanaopita matatizo na kuhitji msaada.
·         Tumefanikisha kuimarisha ushirikiano na taasisi za ndani za kidini, kijamii na kielimu.
·         Tumefanikiwa kujenga uhusiano wenye faida za taasisi za nje ya chuo ndani ya nchi ikiwemo vyuo vikuu vya afya, taasisi ya vyuo vikuu kitaifa (TAHLISO).
Japo tumekuwa tunafaidi matunda ila hatujalipa ada hivyo serikali ijayo ilipe ada.
·         Zaidi, tumesimamia umaliziwaji wa zoezi la uandikishi wa vitambulisho vya taifa na vitambulisho vya kupigia kura.
·         Zaidi, tumemalizia Mabadiliko ya katiba mpya ya taasisi yetu, MUHASSO.
·         Tumefanikiwa kuandaa Muhasso Outreach Event ambapo Serikali ikishirikiana Taasisi za kielimu tumefanya Screening katika kituo cha watoto yatima na kutoa mahitaji ya kijamii kama vile chakula na fedha.
·         Tumefanikiwa kufanya utafiti mdogo juu ya mitazamo wa wanafunzi kuhusu kuwatembelea washauri wao wa masomo.(Academic Mentors). Hii imetoa picha halisi kwa Chuo na MUHASSO ili kwa pamoja tuungane kuitimiza adhma kielimu.


CHANGAMOTO
Ndugu wanamuhasso,
Kama serikali, tukiwa katika mafanikio hayo, tumekumbana pia na changamoto ambazo naamini ndipo serikali ijayo au wanamuhasso tunatakiwa kuongeza juhudi na ushirikiano ili kuipa nguvu serikali katika kutimiza majukumu yake:-
                      i.            Muitikio mdogo wa sisi wanafunzi katika maswala yanayotugusa moja kwa moja na pale serikali inapohitaji nguvu ya pamoja toka kwa wanamuhasso. Hii ni pamoja na kuwa na wanaharakati wanalaumu pekee pasipo kuwa washauri wa serikali katika kutimiza majukumu kwa maslahi ya Muhasso.,
                    ii.            Ufinyu wa mapato ya serikali,MUHASSO husababisha mipango mingine kukwama. Mfano swala la kununua basi lingeanza kwa fedha za ndani tu.
                  iii.            Kutopata majibu au utekelezaji wa haraka wa maswala yetu toka chuo pia llikuwa ni changamoto kwetu kama serikali.MUHASSO. Mfano swala la matengenezo, uboreshaji WIFI na kikao kati yetu na Utawala wa Chuo.
                  iv.             Kutokujali kwa Utawala wa chuo juu ya maswala ya makazi ya wanafunzi haswa katika hosteli za chole. Hii imepelekea wengi kukosa fursa ya kuishi huko.


SHUKRANI
Kwa niaba ya serikali ya wanafunzi, MUHASSO 2015/16 napenda kutoa shukrani zangu kwa ofisi za utawala wa chuo, MUHAS kwa ushirikiano waliotuonyesha katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wangu kama rais wa MUHASSO. Pia nawashukuru watendaji wa ofisi ya afisa Mikopo (Mr F. Kaduma) na ofisi ya mshauri na huduma za wanafunzi na kipekee nimshukuru aliyekuwa Mshauri wa wanafunzi (Dr, CV Kakoko).
Kwa moyo wa upendo, namshukuru sana makamu wangu wa rais, Mr Adam Likiliwike kwa kufanya nae pamoja kwa kuelewana na kushauriana na shukrani za pekee zifike kwa Baraza langu la Mawaziri, 2015/2016 maana pasipo kujitoa kwao mafanikio yasingepatikana hakika. Nawashukuru viongozo wa shule zote tano, wamefanya kazi nzuri katika maswala ya kiakademia pamoja nami. Bila kuwasahau wabunge wote na ofisi ya spika, MUHASSO kwa kuikosoa, kuishauri na kuisaidia serikali hii kufanikisha ahadi zake kwa wanamuhasso.
Mwisho lakini si kwa umuhimu, nawashukuru sana wanamuhasso wote walionisapoti, walionitia moyo, kunishauri na muhimu zaidi kuniombea wakati tunapitia nyakati ngumu kama serikali.
Kwa mwaka mmoja wa kuongoza wasomi, nimejifunza mengi na nimekuwa mtu bora zaidi na mwenye kujinoa zaidi kiuongozi. Naamini huu hautakuwa mwisho bali ndio mwanzo mzuri wa kutumikia taifa kiujumla wake.
Zaidi nawashukuru wote walioniamini na kunipa kura zao hata wale walionipa changamoto wakati wa utendaji nawashukuru sana maana mmeifanya serikali kufanya zaidi.
Imani yenu kwangu haikuwa ya makosa, zaidi imenipa ujasiri,nguvu na kiu ya kutumikia taifa na watanzania kwa ujumla miaka michache hapo mbeleni.
Kwa niaba ya Serikali ya wanafunzi, MUHASSO
Nawasilisha
Mathew B. Mandawa
Rais, Mstaafu – MUHASSO.
2015/2016

                                              ………NAWAPENDA  NYOTE……………


  SOLIDARITY   FOREVER