Wednesday, 8 August 2018

MISS MUHAS 2018

Mashindano ya Miss MUHAS 2018 kwa mara ya kwanza yakifanyikankatika viwanja vya Chole Hostels Masaki. Hii ni kumtamfta mrembo wa Chuo cha Afya Muhimbili

JAKAYA KIKWETE CARDIAC INSTITUTE

TAARIFA KWA MADAKTARI NA WAGONJWA NCHINI

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inapenda kuwajulisha watanzania kuwa kwa kushirikiana na wataalam kutoka nchini Marekani (Madaktari Afrika) “electro physiologist” (EP) tunatarajia kufanya kambi maalum ya magonjwa ya moyo yatokanayo na mfumo wa umeme wa moyo usiofanya kazi sawasawa. Matibabu yatakayotolewa katika kambi hiyo inatarajia kuanza tarehe 11 hadi 18 Agosti 2018 ni pamoja na kuwawekea wagonjwa Pacemakers, ICDs, CRT-Ds na CRT-Ps kutokana na ugonjwa utakaogundulika.

Taasisi inawaomba madaktari wote wa Hospitali za Rufaa nchini kuwaleta wagonjwa wenye matatizo yafuatayo kwa ajili ya matibabu:

Atrioventicular block

Chronic bifascicular and tri fascicular block

Sinus node dysfunction

Complete Heart block

Tachyarrhythmias

Third degree block

Heart Failure with severe LV dysfunction (LBBB) >130m/s

Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na Dkt. Peter Kisenge kwa namba 0713 236 502 na +255 22 2151379 ambaye atawaelekeza utaratibu wa kuwatuma wagonjwa hao.

Imetolewa na:

Kitengo cha Uhusiano
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
06/08/2018