MUHIMBILI UNIVERSITY OF HEALTH AND ALLIED SCIENCES
STUDENTS’ ORGANISATION
MUHASSO
SERIKALI YA WANAFUNZI, MUHASSO 2015/2016.
RIPOTI YA SERIKALI YA WANAFUNZI, MUHASSO
2015/2016.
Ndugu WanaMuhasso..
Kwanza, Napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa
neema yake ya uhai na pumzi anayotupa mpaka saa hii unasoma ripoti hii ya
serikali ya wanafunzi, MUHASSO.
Tukiwa tunafika mwishoni mwa dhamana ya
uongozi mliotupa kwa kura zenu ili kuiongoza taasisi yetu ya jumuiya ya
wanafunzi, MUHASSO. Binafsi kama rais
napenda niwakumbushe kidogo na kutoa mrejesho wa kazi mlionipa kwa mwaka mmoja
kama kiongozi wenu katika utumishi wa kuiongoza Jumuiya hii ya wasomi.
SABABU ZILIZONISUKUMA KUGOMBEA URAIS WA
MUHASSO 2015 – 2016.
Hii ni kuwakumbusha
wanaMuhasso wote walioniamini na kunipigia kura hata wale ambao hawakunipigia
kura ila walinipa ushirikiano baada ya kutangazwa mshindi 18/4/2015 kuwa rais
mpya wa serikali ya wanafunzi, MUHASSO.
Zifuatazo ndizo
sababu zilizonisukuma kama mmoja wa wanamuhasso lakini kwa wakati huo nikiwa
waziri wa mahusiano, sera, utawala bora, jinsia na mambo ya nje katika serikali
ya rafiki yangu katika siasa na uongozi Rais wa awamu ya kwanza- MUHASSO mpya.
1: Muono wangu na
falsafa ninayoiamini juu ya Muhasso mpya
itakayokuwa na umoja na hivyo kuipa nguvu serikali ya wanafunzi, MUHASSO ili
kwa kushirikiana kutatua changamoto mbalimbali zilizokuwa zinatukabili. Na hapo
ndipo nilipokuja na motto wa “Solidarity Forever…”
2: Kiu ya
mabadiliko katika mifumo ya serikali ya wanafunzi, MUHASSO na uendeshaji wa
shughuli zake za kutetea, kusimamia na kuwasemea kwa niaba kama daraja kwa
utawala wa chuo ili kuhakikisha ustawi wa kila mwanamuhasso unalindwa na
kuheshimiwa.
3: Sifa za
kiuongozi na uongozi binafsi nilizotaka kuzitumia ili kutumikia jamii ya wasomi
wenazangu. Kujiamini, ukweli, ujasiri, uelewa binafsi, kujitoa na upendo kwa
watu ni kati ya sifa zilizonisukuma kuzitumia katika nafasi hii kubwa ya
utumishi katika serikali.
Kutokana na sababu hizo
ndipo pamoja na mgombea mwenza wangu, Mr Adam Likiliwike tukaingia katika
kinyang’anyiro cha kugombea na kwa sapoti toka kwa rafiki na wanafamilia wa
Muhasso tukafanya kampeni tukiwa na sera zetu zifuatazo ambazo zilitupa
kuaminika na kushinda uchaguzi huo na kuapishwa 24/04/2015:-
SERA 1: Kuunda serikali ya umoja yenye
uwakilishi wenye uwiano na kupunguza gharama ya uendeshaji wa serikali.
·
Kuunda
serikali yenye kujali uwiano wa kishule, kikozi, kidarasa na kijinsi.
·
Kuondoa/kupunguza
gharama zisizo na ulazima za kuendesha
serikali kwa kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri.
SERA 2: Kuweka mifumo yenye tija katika
maswala ya Elimu.
·
Ushiriki
wa Serikali ya wanafunzi katika uundwaji wa Prospectus na Almanac ya Chuo na
kutupa uwakilishi wa kuwasilisha maoni na mapendekezo yetu.
·
Kuweka
mazingira stahiki ya kusomea na kujifunza ikiwemo kufuatilia utengenezaji wa
vifaa kazi kama maiki, spika, projectors na mazingira bora kusomea katika
maeneo ya NLHs, 24 Halls na Library kwa kuhakikisha uwepo wa soketi zinazofanya
kazi, feni/AC katika vyumba vya mikusanyiko,
·
Kuondoa
tatizo la mwingiliano wa ratiba iliyopelekea wanafunzi kusoma kwa shida pale wanapolazimika
kuhama au kuhairisha vipindi wengine wanapohitaji darasa.
·
Kuhakikisha
matokeo yanatolewa mapema zaidi na kuwekwa katika mfumo ulio imara wa SARIS
inaweza kuonyesha alama Sahihi na GPA ya kila mwanafunzi.
·
Kuhakikisha umalizikaji wa urekebishaji wa
viwango vipya vya fedha ya mahitaji maalumu viendane na mahitaji na kuanza
kutumiwa rasmi na sisi.
·
Kuweka mpango bora unaofaa wa namna ya kulipia
na kufuatilia utunzaji wa nguo zetu za upasuaji(Theatre Attire).
·
Kufuatilia
ufanyaji wa mitihani ya marudio(Supplementary) kwa wanafunzi wa mwaka wa
watatu, wanne na watano kipindi cha likizo ndefu ya 2015.
SERA 3: Marekebisho ya mfumo wa kufuatilia na
kuratibu maswala ya Mikopo na Ruzuku.
·
Kuanzisha
mfumo mpya wa kusaini wenye kutumia muda mfupi bila kuathiri ratiba zetu za
kimasomo.
·
Kufuatilia
kwa kina na ukaribu sio kuulizia ili kuhakikisha pesa zinawafikia wanafunzi kwa
wakati. Hii itaenda sawia na kusaini mapema hata kabla ya siku 70 kuisha ili
kufanikisha kupata pesa kwa wakati.
·
Kufuatilia
taratibu za usainishwaji wa wanafunzi wapatao ruzuku ili kuondoa sintofahamu
juu ya wanaostahili kupewa ruzuku ili kuondoa maswali ya wafaidika.
·
Kushirikiana
na Chuo na wanafunzi wote waliokosa
mikopo ili waweze kupatiwa mikopo yao katika mwaka mpya wa masomo 2015/2016.
SERA 4: Usimamizi mzuri wa maswala ya huduma
za chakula(Cafeteria) na uboreshwaji wa huduma za Afya.
·
Uhusika
wa karibu wa serikali ya wanafunzi, MUHASSO katika upatikanaji wa mtoa huduma
wa Cafeteria. (Tenderer)
·
Kusimamia
kwa makini mikataba wa mtoa huduma ili kuhakikisha huduma bora, yenye usafi na
ya gharama nafuu inatolewa kwa wanamuhasso na hii itakwenda sambamba na kuwepo
kwa timu maalum ya wanamuhasso watano
watakaokuwa wanasimamia kikamilifu(Food Testors).
·
Kuondoa
foleni Chole kwa kuwa na sehemu mbili za kutolea huduma ili kutokuwa na
upotezaji wa muda katika foleni za kupata huduma hizo.
·
Kuwepo
kwa kadi za Bima ambazo haziishi muda wake kabla ya zingine kutoka na kugawiwa
kwa wanafunzi na hivyo kuhakikisha tarehe ya kufikia mwisho(Expiry date)
kusogezwa mbele ili kumpa mtumiaji uhuru wa kutumia popote wakati wowote ili
kutomlazimu kutibiwa MNH pekee kipindi cha mwanzo
SERA 5: Uboreshaji wa huduma za makazi na
Usalama kwa wanafunzi.
·
Utafutaji
wa hosteli mbadala zenye gharama nafuu ili kupunguza uhaba wa makazi miongoni
mwa wanaMuhasso na hii itakuwa sambamba na kuuomba utawala wa chuo kutuchangia
kidogo ili kutomuumiza mwanafunzi kwa malipo makubwa.
·
Ufuatiliaji
wa matengezo ya hosteli zetu kufanyika kwa wakati ili kuweka mazingira salama
kwa wanamuhasso.(milango, mapazia, komeo,vioo, viti, meza)
·
Kuhakikisha
usafi unafanyika kikamilifu ndani na nje ya hostel ili kufanya wanamuhasso
kuishi katika mazingira safi kwa afya zao.
·
Usalama,
kuhakikisha kunakuwepo kwa vifaa vya zima moto(functional fire extinguishers)
na wakazi wa hosteli wanapatiwa mafunzo
ya kuzima moto.
SERA 6: Kuamsha ari ya ushiriki wa
wanamuhasso katika michezo na Burudani.
·
Kuhakikisha
upatikanaji wa vifaa vyote muhimu kwa timu zote ili kuwezesha timu hizo kuwa na
mazoezi ikiwemo jezi,mipira, first aid kits.
·
Kufanyika
kwa mechi mbalimbali ndani na nje ya MUHAS, uwepo wa MUHASSO ligi na bonanza za
michezo mbalimbali za ndani.
·
Kuandaa
matukio ya ufumbuzi wa vipaji vya wanamuhasso
yaani Talents Show.
·
Kutengeneza
Pool table ya Chole ili iweze kutumika ikiwa katika ubora wake ili kuwapa
wanamuhasso pumziko la kiakili.
·
Kuwepo
kwa TV nje ya Cafeteria ili kuondoa msongamano katika ukumbi wetu wa ndani.
SERA 7: Uboreshaji wa mifumo ya kutoa habari,
huduma za mitandao na Intaneti(WiFi).
·
Ufualiaji
na kuhakikisha uwepo na upatikanaji wa WIFI imara yenye nguvu katika hosteli(Chole
na kampusi kuu) zetu na zaidi maeneo ya kusomea(NLHs/24 Hall).
·
Kuimarisha
mfumo mmoja wa kiserikali wa utoaji taarifa kupitia njia zote zifaazo kwa
kuziimarisha kama vile mbao za matangazo, Muhasso facebook pages, Muhasso
blogs, Push - Sms na mitandao ya wasapu.
·
Kuzipa
mamlaka wizara mbalimbali kutoa taarifa zake kwa ufanisi pasipo kuingiliwa na
ofisi za mamlaka ya usimamizi.
·
Kuhakikisha
wanamuhasso wote wananufaika na huduma
zote za vyuo vikuu za mitandao ya simu (University offers) kama vile TIGO. VODA
na AIRTEL.
SERA
8: Uimarishaji wa uwekezaji na kuongeza mapato ya serikali ya wanafunzi,
MUHASSO.
·
Kuipitia
mikataba yote kwa umakini ili tuweze kuitumia kukusanya mapato yetu kikamilifu
na kuongeza mapato ya serikali.
·
Kuichukua
Muhasso stationery na kuiendesha wenyewe ili kupunuza gharama za serikali
kununua huduma hizo ambazo huleta gharama kubwa kwa serikali.
·
Kuanzisha
miradi mingine ya kuongeza mapato ikiwemo ufunguaji wa Saloon katika hostel za
Chole.
SERA 9: Upatikanaji wa usafiri wa uhakika kwa
wanafunzi.
·
Serikali
itaandaa proposo mbalimbali kwa mashirika na watu binafsi ili kukusanya pesa
kwa ajili ya kununua basi moja kwa kuanzia kwa ajili ya kuhakikisha huduma ya
usafiri inapatikana kwa wanamuhasso haswa wakazi wa chole. Serikali itatenga
Tsh Milioni kumi(10m) kama kianzia ambayo imetoka katika mradi mmoja wa
MUHASSO.
SERA 10: Kuimarisha uhusiano wa ndani na nje wa serikali, MUHASSO.
·
Kuanzisha
mfuko maalum wa kusaidia wanafunzi wenye uhitaji wa dharura
·
Kuimarisha
ushirikiano na taasisi za ndani za kidini, kijamii na kielimu.
·
Kujenga
uhusiano wenye faida za taasisi za nje ya chuo ndani ya nchi na nje ya nchi
pia.
MAFANIKIO YA SERIKALI YA WANAFUNZI, MUHASSO
2015/2016.
Ndugu wanamuhasso,
Baada ya kujinadi
kwa dhati na kwa kujiamini ili kuweza kuleta mabadiliko makubwa yaliyotegemewa
na mamia ya wanamuhasso katika 2015/2016. Yafuatayo yamefanyika na kufanikiwa
kama ambavyo niliyaahidi pamoja na Makamu wangu wa rais:-
SERA 1: Kuunda serikali ya umoja yenye
uwakilishi wenye uwiano na kupunguza gharama ya uendeshaji wa serikali.
·
Tumefanikiwa
kuunda serikali yenye kujali uwiano wa kishule, kikozi, kidarasa na kijinsi
sawa sawa na matakwa ya kikatiba na hii imeimarisha umoja na upendo wetu.
Ofisi ya rais – MDs
Ofisi ya waziri mkuu - BPharm na Public health.
Mawaziri – MDs 5, Bpharm- 1, Public health – 1, BscN-1 and
DDS -1.
Naibu mawaziri - MDs 9, Bpharm- 3,
Public health – 1,BscN-1 and DDS -1.
·
Tumepunguza
ukubwa wa serikali (Executive) kwa nafasi 10 pungufu kulinganisha na ilivyokuwa
mwanzo na hii imepunguza matumizi ya pesa za wanamuhasso katika gharama za
kuendesha serikali na kuwekeza zaidi katika huduma za pamoja.
SERA 2: Kuweka mifumo yenye tija katika
maswala ya Elimu.
·
Serikali
imeshiriki kwa kukusanya maoni na mapendekezo toka kwa wanafunzish iriki juu
uundwaji wa Prospectus na Almanac LAKINI bado tulikutana na Ugumu katika
kuelewana juu ya kuondolewa kwa sheria ya Sapu 3 na muda wa kufanya sapu wakati
wa likizo ndefu.(clinical rotations)
Japo sheria hii haijatoweka kabisa
lakini imepunguzwa kutotumika kwa mwaka
wa pili wa kozi zote za miaka mitatu ( BMLS, BRRT na BScEnv ).
·
Serikali
imehakikisha kuwepo kwa matengenezo ya
vifaa kazi kama maiki, spika, projectors na kuhahakisha mazingira bora kusomea
katika maeneo ya NLHs, 24 Hall na Library kwa kuhakikisha uwepo wa soketi
zinazofanya kazi na feni/AC.
·
Tumehakikisha
tatizo la muingiliano wa ratiba limepungua kwa kiasi kikubwa kulinganisha na
hapo awali kwa kuwa na ratiba kuu inayoonyesha madarasa kwa kupishana.(Central
timetable)
·
Tumehakikisha
matokeo yanatolewa mapema zaidi na imewapa fursa ya kujiandaa kwa mitihani ya
marudio (supplementaries) na kuanza mafunzo mapema (internship) kwa waliohitimu.
·
Kuanzishwa kwa mfumo wa kuonyesha GPA ya kila
mwanafunzi katika akaunti za ‘SARIS’
·
Tumehakikisha urekebishaji wa viwango vipya
vya fedha ya mahitaji maalumu umefika bodi ya mikopo na kufanyiwa kazi katika
kipindi cha bajeti 2016/17. Na hii itatoa fursa ya kuanza kutumika kwa mwaka wa
kwanza wapya wa 2016/2017.
·
Tumeweka mpango bora wa kulipia na kufuatilia
utunzaji wa nguo zetu za upasuaji (Theatre Attire) ambapo wale mwaka wa tatu pekee ndio watakuwa wanalipia
ununuzi wa nguo hizo.
·
Tumefanikiwa
kusaidia kufanyika kwa mitihani ya marudio (Supplementary) kwa wanafunzi wa
mwaka wa watano(MD5X) kipindi cha likizo ndefu ya oktoba 2015.
SERA 3: Marekebisho ya mfumo wa kufuatilia na
kuratibu maswala ya Mikopo na Ruzuku.
·
Tumefanikiwa
kuanzisha mfumo mpya wa kusaini wenye kutumia muda mfupi bila kuathiri ratiba
zetu za kimasomo.
·
Tumefanikiwa
kuhakikisha na kufuatilia kwa kina na ukaribu na kupelekea pesa kuwafikia
wanafunzi kwa wakati.
Japo
kumekuwa na changamoto kwa bumu la april, 2016 na pesa za disemba, 2015 za BS, SFR na PT zilichelewa kwa sababu
zilizokuwa nje ya MUHASSO.
·
Tumefanikiwa
kusimamia taratibu za usainishwaji wa wanafunzi wapatao ruzuku na hii imeondoa
sintofahamu juu ya wanaostahili kupewa ruzuku.
·
Tumeshirikiana
na Chuo na wanafunzi wote waliokosa mikopo
2014/2015 na wameweza kupatiwa mikopo katika mwaka 2015/2016.
SERA 4: Usimamizi wa maswala ya huduma za
chakula(Cafeteria) na uboreshwaji wa huduma za Afya.
·
Serikali,
tumefanikiwa kushiriki kikamilifu na karibu katika upatikanaji wa mtoa huduma mpya wa Cafeteria kwa kulinda maslahi ya wanafunzi
wake.
·
Tumemezidi
kusimamia kwa makini mkataba wa mtoa huduma ili kuhakikisha huduma bora,usafi
na ya gharama nafuu sawaia na mkataba wake
inatolewa.
·
Serikali
tumekubaliana na ofisi za NHIF- Ilala juu ya mfumo wa kutoa kadi za Bima wakati
tu tunavyofanya usajili chuoni ili kumpa mwanafunzi mtumiaji uhuru wa kutumia
popote wakati wowote ili kutomlazimu kutibiwa MNH pekee kipindi cha mwanzo kama
ilivokuwa mwanzoni. Kadi zilizopo zitatumiwa mpaka tutakapopata mpya katika
mwaka mpya ujao wa masomo.
·
Zaidi,
tumehakikisha chanjo dhidi ya homa ya Ini (HEPATITIS VACCINATION) imetolewa kwa
wanamuhasso wote waliokuwa tayari.(1209 wamepatiwa chanjo hiyo)
SERA 5: Uboreshwaji wa huduma za makazi na
Usalama kwa wanafunzi.
·
Serikali
ilifanikiwa kupata hosteli mbadala ili kupunguza uhaba wa makazi miongoni mwa
wanaMuhasso lakini muitikio wa wanafunzi ulikuwa mdogo hivyo zikachukuliwa na vyuo
vingine.
Japo
,MUHASSO tulifikia hatua nzuri LAKINI juhudi zetu hazikuzaa matunda baada ya
chuo kudai hakiwezi kutuchangia gharama ya malazi.ya wanafunzi.
·
Tumezidi
kufuatilia matengezo ya hosteli zetu kufanyika kwa wakati ili kuweka mazingira
salama kwa wanamuhasso.(milango, mapazia, komeo,vioo, viti, meza)
Japo
haijafikia kiwango tulichotegemea kwa sababu zilizotolewa na Chuo kutokuwa na
fedha za kukamilisha matengenezo yote HATA HIVYO bajeti ya kutosha imetengwa
kwa ajili ya ukarabati huu wakati wa likizo ijayo.
·
Tumehakikisha
usafi unafanyika kikamilifu ndani na nje ya hostel ili kufanya wanamuhasso
kuishi katika mazingira safi kwa afya zetu.
·
Usalama,
tumefanikiwa kuhakikisha wanamuhasso wakazi wa hosteli wamepatiwa mafunzo ya
kuzima moto na vifaa vya kuzimia moto vinavyofanya kazi vipo katika hosteli
zote.
·
Zaidi,
tumefanikisha kuhakikisha ulinzi umeimarishwa haswa baada ya matokeo ya wizi
kutokea.
·
Tumehakikisha
dawa za kuua wadudu zinapigwa katika hostel zetu na chuo kilitoa ushirikiano
mzuri katika eneo hili.
SERA 6: Kuuhisha ushiriki wa Wanamuhasso katika
michezo na Burudani.
·
Tumefanikiwa
kucheza mechi mbalimbali ndani na nje ya MUHAS.
·
Tumefanikiwa
kuandaa MUHASSO ligi ambapo mwaka wa pili walitwaa kombe
·
Tumefanikiwa
kuandaa na kushiriki bonanza za michezo mbalimbali. Mfano: Tigo bonanza
·
Tumeandaa
matukio ya ufumbuzi na kuonyesha vipaji vya wanamuhasso yaani TALENTS SHOWs. (Juni,2015
na march, 2016)
·
Tumefanikiwa
kununua na kutoa vifaa vyote muhimu vya michezo kwa timu zote ili kuwezesha
timu hizo kuwa na mazoezi.(football, volleyball, basketball)
·
Tumetengeneza
Pool table ya Chole.
·
Tutakuwa
na TV katika Cafeteria ili kuondoa msongamano katika ukumbi wetu wa ndani. (Shukrani
kwa mzabuni wetu wa cafeteria, hatua za mwisho zinafanyika ili ifungwe ndani ya
Cafeteria yetu).
SERA 7: Uboreshaji wa mifumo ya kutoa habari,
huduma za mitandao na Intaneti (WiFi).
·
Tumefanikiwa kuhakikisha uwepo na upatikanaji
wa WIFI yenye nguvu katika hosteli(Chole
na M. Campus)haswa maeneo ya kusomea(NLHs/24 Hall/New Cafeteria-Chole).
Japo
bado haijawa imara kutokana na uchache wa vifaa unganishi.
·
Tumeonyesha
mfano uliosifika katika mfumo wa kiserikali wa utoaji taarifa kupitia njia zote
zifaazo kwa kuziimarisha kama vile mbao za matangazo, Muhasso facebook pages,
Muhasso blogs, Push - Sms na mitandao ya wasapu na telegram.
·
Serikali
imeonyesha mgawanyo wa madaraka kiutendaji kwa wizara mbalimbali kutoa taarifa
zake kwa ufanisi pasipo kuingiliwa na ofisi za mamlaka ya usimamizi.
·
Tumesimamia
uungwanishaji katika huduma zote za vyuo vikuu za mitandao ya simu (University
offers) kama vile TIGO, HALOTEL,VODA na AIRTEL.
SERA
8: Uimarishaji wa Uwekezaji na kuongeza mapato ya serikali ya wanafunzi,
MUHASSO.
·
Tumefanikiwa
kuipitia mikataba na kusimamia ukusanyaji wa mapato yetu kikamilifu. Hii imekuwa sambamba
na kubadili mtoa huduma katika Saluni yetu ili kuboresha huduma zake.
·
Tumefanikiwa
kununua vifaa vyetu wenye vya huduma za kisteshenari na kupunguza gharama za
serikali kununua huduma nje.
SERA 9: Upatikanaji wa usafiri wa uhakika kwa
wanafunzi.
·
Tumefanikiwa
kuandaa proposals na kuzisambaza kwa mashirika na watu binafsi kama vile bank
(NMB,CRDB), makampuni ya simu (TIGO, AIRTEL, VODA) na makampuni binafsi
(IPPL-Dr. Mengi, QGL- Mr Manji, MeTL- Mr Dewji).
Japo majibu bado sio mazuri mpaka
sasa. Ufuatiliaji kwa serikali mpya uendelee.
·
Serikali
imekusanya na kutenga Tsh Milioni kumi (10m) kama kianzio ambayo imetoka katika
mradi mmoja wa MUHASSO.
.
SERA 10: Kuimarisha Uhusiano wa Ndani na Nje wa serikali, MUHASSO.
·
Tumefanikiwa
kuanzisha mfuko maalum wa dharura kwa ajili ya kusaidia wanamuhasso wanaopita
matatizo na kuhitji msaada.
·
Tumefanikisha
kuimarisha ushirikiano na taasisi za ndani za kidini, kijamii na kielimu.
·
Tumefanikiwa
kujenga uhusiano wenye faida za taasisi za nje ya chuo ndani ya nchi ikiwemo
vyuo vikuu vya afya, taasisi ya vyuo vikuu kitaifa (TAHLISO).
Japo tumekuwa tunafaidi matunda ila
hatujalipa ada hivyo serikali ijayo ilipe ada.
·
Zaidi,
tumesimamia umaliziwaji wa zoezi la uandikishi wa vitambulisho vya taifa na vitambulisho
vya kupigia kura.
·
Zaidi,
tumemalizia Mabadiliko ya katiba mpya ya taasisi yetu, MUHASSO.
·
Tumefanikiwa
kuandaa Muhasso Outreach Event
ambapo Serikali ikishirikiana Taasisi za kielimu tumefanya Screening katika kituo cha watoto yatima na kutoa mahitaji ya kijamii
kama vile chakula na fedha.
·
Tumefanikiwa
kufanya utafiti mdogo juu ya mitazamo wa wanafunzi kuhusu kuwatembelea washauri
wao wa masomo.(Academic Mentors). Hii imetoa picha halisi kwa Chuo na MUHASSO
ili kwa pamoja tuungane kuitimiza adhma kielimu.
CHANGAMOTO
Ndugu wanamuhasso,
Kama serikali, tukiwa katika mafanikio hayo, tumekumbana pia na
changamoto ambazo naamini ndipo serikali ijayo au wanamuhasso tunatakiwa
kuongeza juhudi na ushirikiano ili kuipa nguvu serikali katika kutimiza
majukumu yake:-
i.
Muitikio
mdogo wa sisi wanafunzi katika maswala yanayotugusa moja kwa moja na pale
serikali inapohitaji nguvu ya pamoja toka kwa wanamuhasso. Hii ni pamoja na
kuwa na wanaharakati wanalaumu pekee pasipo kuwa washauri wa serikali katika
kutimiza majukumu kwa maslahi ya Muhasso.,
ii.
Ufinyu
wa mapato ya serikali,MUHASSO husababisha mipango mingine kukwama. Mfano swala
la kununua basi lingeanza kwa fedha za ndani tu.
iii.
Kutopata
majibu au utekelezaji wa haraka wa maswala yetu toka chuo pia llikuwa ni
changamoto kwetu kama serikali.MUHASSO. Mfano swala la matengenezo, uboreshaji
WIFI na kikao kati yetu na Utawala wa Chuo.
iv.
Kutokujali kwa Utawala wa chuo juu ya maswala
ya makazi ya wanafunzi haswa katika hosteli za chole. Hii imepelekea wengi
kukosa fursa ya kuishi huko.
SHUKRANI
Kwa niaba ya
serikali ya wanafunzi, MUHASSO 2015/16 napenda kutoa shukrani zangu kwa ofisi
za utawala wa chuo, MUHAS kwa ushirikiano waliotuonyesha katika kipindi cha
mwaka mmoja wa uongozi wangu kama rais wa MUHASSO. Pia nawashukuru watendaji wa
ofisi ya afisa Mikopo (Mr F. Kaduma) na ofisi ya mshauri na huduma za wanafunzi
na kipekee nimshukuru aliyekuwa Mshauri wa wanafunzi (Dr, CV Kakoko).
Kwa moyo wa upendo,
namshukuru sana makamu wangu wa rais, Mr Adam Likiliwike kwa kufanya nae pamoja
kwa kuelewana na kushauriana na shukrani za pekee zifike kwa Baraza langu la
Mawaziri, 2015/2016 maana pasipo kujitoa kwao mafanikio yasingepatikana hakika.
Nawashukuru viongozo wa shule zote tano, wamefanya kazi nzuri katika maswala ya
kiakademia pamoja nami. Bila kuwasahau wabunge wote na ofisi ya spika, MUHASSO
kwa kuikosoa, kuishauri na kuisaidia serikali hii kufanikisha ahadi zake kwa
wanamuhasso.
Mwisho lakini si
kwa umuhimu, nawashukuru sana wanamuhasso wote walionisapoti, walionitia moyo,
kunishauri na muhimu zaidi kuniombea wakati tunapitia nyakati ngumu kama
serikali.
Kwa mwaka mmoja wa
kuongoza wasomi, nimejifunza mengi na nimekuwa mtu bora zaidi na mwenye kujinoa
zaidi kiuongozi. Naamini huu hautakuwa mwisho bali ndio mwanzo mzuri wa
kutumikia taifa kiujumla wake.
Zaidi nawashukuru
wote walioniamini na kunipa kura zao hata wale walionipa changamoto wakati wa
utendaji nawashukuru sana maana mmeifanya serikali kufanya zaidi.
Imani yenu kwangu
haikuwa ya makosa, zaidi imenipa ujasiri,nguvu na kiu ya kutumikia taifa na
watanzania kwa ujumla miaka michache hapo mbeleni.
Kwa niaba ya
Serikali ya wanafunzi, MUHASSO
Nawasilisha
Mathew B. Mandawa
Rais, Mstaafu – MUHASSO.
2015/2016
………NAWAPENDA NYOTE……………
SOLIDARITY FOREVER